Kinara wa DCP Righathi Gachagwa sasa anamtaka Rais wa Marekani Donald Trump kufanya uteuzi wa balozi ambaye hana mapendeleo kwa utawala wa Rais Ruto.
Gachagua akiwa katika mahojiano jijini Kansas,Amerika,anasema kuwa Rais Trump atasaidia pakubwa katika ukombozi wa taifa la Kenya iwapo atateua balozi ambaye hana mapendeleo.
Kulingana na Gachagua Rais Trump anastahili kumtuma balozi ambaye anatajriba kama Smith Hempstone,ambaye aliwahi kuhudumu nchini kati ya 1989-1993 kwani alikuwa miongoni mwa walioshinikiza kukumbatiwa kwa mfumo wa vyama vingi katika uchaguzi mkuu wa 1992.
Kinara huyo anadai kuwa Rais Ruto ameshiriki pakubwa katika ukiukaji wa haki za kibinadamu,aidha alijipigia debe kwamba akichaguliwa kuwa rais 2027,maafisa waliousika kwa mauaji ya vijana watakamatwa na kufunguliwa mashtaka,vile vile alisema kuwa akipata uongozi huo atafidia familia ya vijana waliouawa.
By Barasa Saenyi