Kesi ya kuwatimua majaji sita akiwemo jaji mkuu Martha Koome imetupiliwa mbali na tume ya huduma za mahakama JSC kwa kutotimiza vigezo vya katiba.
Aliye kuwa rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Nelson Havi,Edwin Dande ambaye ni mwanabiashara,Victoria Naishorua na kampuni ya Benjoh Amalgamated and Muiri Coffee Estate,ndio walalamishi.

Havi alimtuhumu jaji mkuu Martha Koome kwa kuteua jopo la majaji watatu kusikiliza kesi ambayo iliwasilishwa didhi ya JSC,na kwamba kibarua hicho kilipaswa kutekelezwa na watu wengine.
JSC kwa upande wake ikasema kuwa kulingana na kipengee cha 165(4) cha katiba,Jaji mkuu ndiye pekeeyake aliye na mamlaka ya kuteua majaji wa kusikiliza kesi aina hiyo.
Baada ya kesi hii kusikilizwa kwa muda,mahakama Rufaa imetoa uamuzi wake na kwamba hatua ya koome iliafikia hitaji la katiba na kutupilia mbali madai kuwa Koome aliteua majaji wasio na uzoefu.
By Joel Esabu