Huu ndio ulikuwa mtihani wa mwisho wa KCPE kufanywa chini ya mfumo wa 8-4-4 ambao umekuwepo kwa kipindi cha miongo minne iliyopita.
Mfumo huo umepisha rasmi mfumo mpya wa umilisi, CBC.
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anasema jumla ya wanafunzi milioni 1, 406, 557 walifanya mtihani huo ikiwa ni sawa na asilimia 99.34.
Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika Baraza la Kitaifa la Mitihani Nchini, KNEC jijini Nairobi Nov 23. 2023 Alhamisi, Waziri Machogu alisema jumla ya wanafunzi 8,525 walipata kati ya alama 400-500 ikiwa ni sawa na asilimia 0.60.
Wanafunzi 352,782 walipata kati ya alama 300-399 huku 658,278 wakipata alama kati ya 200-209.
Wanafunzi 383,025 walipata alama kati ya 100-199 huku wanafunzi 2,060 wakipata chini ya alama 100.
Wanafunzi wote watajiunga na kidato cha kwanza mwakani huku waliokosa kufanya mtihani wa KCPE mwaka huu wakipewa fursa ya kuufanya tena mwezi Januari mwakani.
Jumla ya wanafunzi 9,000 walikosa kuufanya mtihani huo huku wanafunzi 205 wakituhusiwa kuufanya licha ya kwamba hawakuwa wamesajiliwa.
By Matanda Emmanuel