Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis awasili nchini Kenya, kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu. Kuwasili kwake hapa nchini Jumatatu jioni, ni sehemu ya ziara yake ya mataifa manne barani Afrika.
Kulingana na afisi ya Rais wa Romania, Rais Iohannis anatarajiwa kuzuru Kenya, Tanzania, Cape Verde na Senegal kati ya tarehe 14 na 23 mwezi Novemba.
Ziara hiyo ya Rais wa Romania, ndiyo ya kwanza kufanywa na afisa wa ngazi za juu wa kisiasa na kidiplomasia Barani Afrika, katika muda wa miongo mitatu iliyopita.
Wakati wa ziara hiyo, rais huyo wa Romania atakutana na Rais William Ruto na kuhudhuria mkutano na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa mazingira UNEP, jijini Nairobi.
Nchini Tanzania, kiongozi huyo wa Romania anatarajiwa kushiriki meza ya mazungumzo na Rais wa taifa hilo Samia Suluhu Hassa.
“Ziara hizi zinalenga kufufua uhusiano wa kiuchumi, kutoa fursa mpya za ushirikioano katika maeneo yenya maslahi sawa pamoja na kushughulikia changamoto za kimataifa,”ilisema afisi ya rais wa Romania.
Mwandishi; Neema Faith