Hatua hii inafuatia kupitishwa kwa sheria bungeni inayoruhusu ubinafsishaji wa mashirika ya serikali.
Ubinafsishaji wa mashirika hayo ni mojawapo ya mapendekezo yaliyototolewa kwa serikali ya Kenya na Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF kama njia moja ya kufufua uchumi uliodorora.
Ili kunusuru uchumi wa nchi hii, IMF imetangaza kutoa mkopo wa dola bilioni 12 mwaka ujao kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Shirika hilo aidha limependekeza serikali kuyafanyia mabadiliko mashirika ya Kenya Power na Kenya Airways ambayo yalinakili hasara mwaka jana.
November 24.2023