Kufikia jana Alhamisi, watu 100 waliripotiwa kufariki kutokana na mafuriko huku maelfu ya nyumba zikisombwa au kufunikwa kwa maji ya mafuriko.
Serikali ya Somalia ilitangaza mafuriko kuwa janga la kitaifa mapema mwezi huu.
Mataifa mengi ya upembe wa Afrika yameshudia mafuriko tangu mwezi Oktoba mwaka huu kutokana na mvua kubwa.
Nchini Kenya, mvua kubwa inanyesha kwa sasa na imekuwa chanzo cha mafuriko ambayo yamesababisha maafa, uharibifu wa miundombinu na maelfu ya watu kupoteza makazi.
Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini humo inasema mvua hiyo itaendelea hadi mwezi Januari mwakani.
Serikali ya Kenya nayo pia imetakiwa kutangaza mafuriko yanayoshuhudiwa nchini humo kuwa janga la taifa.