Mshindi wa rekodi ya mbio za marathon humu nchini kelvin kiptum mwenye umri wa miaka 24 anazikwa leo katika uwanja wa riadha wa taifa baada kufariki katika ajali ya gari.

 

coffin of late marathoner Kelvin Kiptum

Rais william ruto na mkuu wa riadha duniani sebastian coe, wanatarajiwa kuwa miongoni mwa watakao hudhuria mazishi katika eneo la rift valley ambapo kiptum alizaliwa.

Kiptum ambaye ni baba wa watoto wawili alifariki mnamo februari 11, miezi michache tu baada ya kuvunja rekodi ya mbio za marathon huko chicago mnamo oktoba, na kuushangaza ulimwengu wa riadha.
Alikimbia kwa muda wa saa mbili na sekunde 35, huku akipunguza sekunde 34 kutoka kwa muda wa kasi uliopita, uliowekwa na mpinzani wake gwiji wa mbio za marathon eliud kipchoge.

Kiptum aliyeshiriki mbio za marathon mara tatu, alishinda zote.

Kifo chake cha ghafla kimeiacha nchi hii, na jamii kubwa ya wanariadha na majonzi, huku mamia ya watu wakijitokeza hapo jana kutoka kijiji alichozaliwa cha chepkorio, magharibi mwa kenya ili kumuenzi nyota huyo anayechipuka ambaye ndiye mshiriki bora wa michezo ya olimpiki ya paris 2024.

Aidha mashabiki na wanariadha kutoka sehemu mbalimbali walijitosa barabarani, wengine wakiwa wamejawa na huzuni, nao wengine wakiimba nyimbo wakati mwili wake ulipokuwa ukisafirishwa hadi iten eneo la bonde la ufa.

Coe, ambaye aliwasili eldoret hapo jana, alionyesha huzuni mwingi kutokana na kifo cha mwanariadha huyo.
“Mafanikio ya kelvin ni ya ajabu. kwamba alijiendeleza na kujiinua akiwa katika umri mdogo, hivyo kweli ni mafanikio ya kipekee,” alisema.