Record Holder Ferdinand Omanyala After Training.

Tuanzie na riadha ambapo bingwa mara nne wa dunia katika mbio za mita elfu moja mia tano, Faith Kipyegon, ameanza msimu kwa kishindo baada ya kushinda mbio za mita elfi tano kwenye mashindano ya Diamond League yaliyofanyika mjini Shanghai, China.
Kipyegon alitumia dakika 14 24.14 na kuweka muda bora zaidi duniani msimu huu katika mbio za wanawake za mita 5,000.
Mkenya huyo aliongoza mbio hizo kutoka mwanzo hadi mwisho akionyesha kiwango bora kilichowavutia mashabiki wengi wa riadha duniani.
Na bado katika mashindano hayo ya Diamond League, mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala aliendelea kung’ara baada ya kumaliza wa pili katika mbio za mita 100.
Omanyala alitumia sekunde 9.98, ikiwa ni mara ya nne msimu huu kukimbia chini ya sekunde 10.
Mshindi wa mbio hizo alikuwa Gift Leotlela wa Afrika Kusini kwa sekunde 9.97 huku Kenneth Bednarek wa Marekani akimaliza wa tatu pia kwa sekunde 9.98.

Faith Kipyegon On a Previous Race Championship.

Kenya premier league
Tukielekea katika soka la humu nchini, Gor Mahia wameikaribia taji la FKF Premier League baada ya kuichapa Murang’a SEAL mabao 3 kwa 1.
Ushindi huo unaifanya Gor Mahia kubaki na pointi mbili pekee kutangaza ubingwa rasmi wa ligi.
Kwingineko, Shabana waliibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Bidco United, matokeo yaliyothibitisha rasmi kushuka daraja kwa Bidco United.
Nao AFC Leopards waliendeleza ubora wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Kakamega Homeboyz.
Katika matokeo mengine, Nairobi United walitoshana nguvu kwa sare ya mabao 2 kwa 2 dhidi ya Posta Rangers huku Mathare United wakipata ushindi muhimu wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Mara Sugar.

England premier league
Tukielekea Ligi Kuu Uingereza, mbio za kuwania ubingwa zinaendelea kushika kasi huku vinara Arsenal wakitarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo dhidi ya Burnley katika uga wa Emirates.
Ushindi kwa Arsenal utaongeza pengo lao kileleni dhidi ya Manchester City.
Matokeo ya hivi karibuni nchini Uingereza:
• Manchester United waliichapa Nottingham Forest mabao 3 kwa 2.
• Newcastle United waliibuka na ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya West Ham United.
• Aston Villa waliwashangaza Liverpool kwa ushindi wa mabao 4 kwa 2.

Nchini Hispania, hakuna mechi za La Liga leo baada ya duru ya 37 kukamilika mwishoni mwa wiki.
Barcelona waliendeleza ubora wao nyumbani baada ya kuifunga Real Betis mabao 3 kwa 1 na kuhakikisha wanamaliza msimu bila kupoteza nyumbani.
Nao Real Madrid waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Sevilla.

Na nchini Ujerumani, msimu wa Bundesliga tayari umekamilika huku Bayern Munich wakimaliza kwa kishindo baada ya kuichapa Köln mabao 5 kwa 1.

 

By Joshua Kiptoo