Kuanza na hapa nyumbani transzoia County, klabu ya Kiminini Combined FC maarufu kama Bazuu Boys imeandika historia baada ya kutwaa ubingwa wa FKF Division One Zone C na rasmi kupanda daraja kwenda National Super League, NSL.Katika mchezo uliochezwa hapa juzi kwenye uwanja wa Eldoret Showground, Bazuu Boys waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya GFE 105 FC.
Nyota wa mchezo alikuwa Gregory Agesa aliyefunga mabao yote mawili na kuhakikisha timu yake inapata ushindi muhimu uliowapeleka moja kwa moja NSL msimu ujao.
Kocha wa timu hiyo Yohana Wanyama amesema ushindi huo umetokana na nidhamu, kujituma kwa wachezaji pamoja na ushirikiano mkubwa kutoka kwa mashabiki waliokuwa bega kwa bega na timu hiyo msimu mzima.Akizungumza hii hapa kauli yake :
“Tunamshukuru Mungu kwa ushindi huu na kwa kutuwezesha kupanda daraja kwenda National Super League. Wachezaji wameonyesha moyo mkubwa wa kupambana msimu mzima na mashabiki wamekuwa nguzo muhimu sana kwetu,” alisema kocha Wanyama.
Kenya premier league
Kwingineko!
Katika Ligi Kuu ya Kenya, mbio za ubingwa zimezidi kupamba moto huku mechi tatu za mwisho zikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.
Gor Mahia watacheza na Murang’a Seal, Mara Sugar pamoja na Nairobi United katika mechi zitakazoamua hatima yao ya ubingwa.
Kwa upande mwingine AFC Leopards watamenyana na Kakamega Homeboyz, APS Bomet na Bidco United wakisaka pointi muhimu za kuendelea kubaki kwenye mbio za kutwaa taji la ligi.
Mashabiki sasa wanasubiri kuona ni timu gani itateleza kwanza katika vita hivi vya kusisimua vya ubingwa wa KPL.Je ni Gormahia au Afc Leopards tegea uhondo kamili hapa ndani ya imani radio .
Na Kimataifa, Ligi Kuu ya England, EPL, inaendelea kushika kasi huku mechi za wiki ya 37 zikitarajiwa kuchezwa Jumapili, Mei 17, 2026, kufuatia pambano la Ijumaa leo usiku kati ya Aston Villa na Liverpool.
Ratiba ya mechi hizo kwa saa za Afrika Mashariki ni kama ifuatavyo:
1) Manchester United watacheza na Nottingham Forest – Saa 8:30 mchana
2) Brentford watamenyana na Crystal Palace – Saa 11:00 jioni
3) Leeds United watacheza na Brighton & Hove Albion – Saa 11:00 jioni
4) Wolverhampton Wanderers watavaana na Fulham – Saa 11:00 jioni
5) Everton watakipiga na Sunderland – Saa 11:00 jioni
6) Newcastle United watavaana na West Ham United – Saa 1:30 usiku
Timu mbalimbali zinapambana kuhakikisha zinamaliza msimu katika nafasi nzuri huku ushindani wa ubingwa na nafasi za juu ukiendelea kushika kasi kati ya vijana wa mikel artata arsenal na ManchesterCity yake pep gadiola.
